Mwenyekiti wa klabu upande wa wanachama, Murtaza Mangungu amemkabidhi zawadi ya jezi Mweka Hazina wa Al Hilal, Farik Yahya Mohammad huku na yeye akimkabidhi ngao kama ishara ya shukrani na kuimarisha mshikamano uliopo baina yetu.
Baada ya kupokea zawadi hiyo, Farik ameushukuru uongozi wa klabu kwa kuonyesha mshikamano huku akisisitiza anaomba usiishie hapa bali uendelee.
“Tunawashukuru kwa ushirikiano mkubwa mliotupatia, tumefurahi kwa zawadi na tunaamini urafiki huu utaendelea baada ya hapa,” amesema Farik.
Al Hilal walitualika kushiriki michuano maalum kwa ajili ya kuandaa timu zetu kuelekea Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika michuano ambayo Timu ya Asante Kotoko ya Ghana ilishiriki.