Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City uliopigwa Uwanja wa Sokoine umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.
Kiungo mkabaji Mzamiru Yassin alitupatia bao la kwanza dakika ya 15 baada ya kumalizia pasi ya kisigino kutoka kwa John Bocco kufuatia krosi iliyopigwa na Clatous Chama.
Baada ya bao hilo tuliendelea kulishambulia lango la City ambapo kama tungeongeza umakini tungeenda mapumziko tukiwa mbele kwa zaidi ya bao moja.
Tariq Seif aliisawazishia City dakika ya 78 ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Awadh Juma na kupiga shuti la chini chini ambalo mlinda mlango Aishi Manula hakuweza kuliokoa.
Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Augustine Okrah (aliyeumia), Bocco na Moses Phiri na kuwaingiza Kibu Denis, Pape Sakho na Habib Kyombo.