Tumegawana pointi na Polisi

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania uliofanyika Uwanja wa Ushirika mjini Moshi umemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu lakini changamoto ikawa kumalizia nafasi zilizopatikana.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kutengeneza nafasi kadhaa huku wenyeji Polisi wakicheza kwa kuzuia zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Yusuf Mhilu, Mzamiru Yassin, Medie Kagere, Rally Bwalya na Erasto Nyoni na kuwaingiza Pape Sakho, Jonas Mkude, Clatous Chama, Bernard Morrison na Jimmyson. Mwanuke.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi 41 tukiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 19.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER