Tumegawana pointi na Namungo

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC uliopigwa Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi umemalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Wenyeji Namungo walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema dakika ya nane lilliofungwa na Jacob Massawe akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Shiza Kichuya.

Baada ya bao hilo tulizidi kuliandama lango na Namungo ambapo dakika ya 31 Kibu Denis alipoteza nafasi ya wazi ya kufunga kufuatia shambulizi kali tulilofanya.

Shomari Kapombe alitufungia bao la kusawazisha dakika ya 41 akimalizia pasi ya Mzamiru Yassin baada ya Kibu kuipisha na kuwahadaa walinzi wa Namungo.

Dakika ya 53 Obrey Chirwa aliipatia Namungo bao la pili kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ralients Lusajo baada ya walinzi wetu kushindwa kuondoa hatari.

Kibu alitusawazishia bao hilo dakika ya 78 kwa shuti kali la chini chini akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa Medie Kagere.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Mzamiru, Peter Banda, Mohamed Hussein na Joash Onyango na kuwaingiza Pape Sakho, John Bocco, Yusuf Mhilu na Pascal Wawa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER