Tumegawana pointi na Namungo Majaliwa

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC uliopigwa Uwanja wa Majaliwa umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku tukishambuliana kwa zamu huku umiliki wa mpira ukiwa zaidi upande wetu.

Jean Baleke alutupatia bao la kwanza kwa shuti la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Saido Ntibazonkiza dakika ya 27.

Hassan Kabunda aliisawazishia Namungo dakika ya 39 baada ya mlinda mlango Ally Salim kukosea kuondoa mpira wa kona uliopigwa na Shiza Kichuya kabla ya kumkuta mfungaji.

Kipindi cha pili kasi ya mpira iliongezeka na kushambuliana kwa zamu lakini ufanisi wa kutumia nafasi ulikuwa mdogo.

X1: Nahimana, Kibailo, Asante, Magingi, Oruchumu, Nyenye (Mwashinga 85′), Kabunda, Domayo, Buswita (Kassim 87′), Masawe (Michael 87:), Kichuya

Walioonyeshwa kadi: Oruchumu 52′

X1: Ally, Israel, Gadiel, Kennedy, Onyango, Erasto, Sakho (Okrah 76′), Kapama (Mkude 56′), Baleke, Ntibazonkiza, Banda (Bocco 84′)

Walioonyeshwa kadi: Ntibazonkiza 76′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER