Tumegawana pointi na mtani

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi watani wetu ya jadi Yanga uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa sare ya bao moja.

Tulianza mchezo kwa kasi ambapo dakika ya kwanza alimanusura Moses Phiri baada ya kukosa mpira wa krosi uliopigwa na Augustine Okrah na kupita katikati ya mstari wa goli.

Okrah alitupatia bao la kwanza dakika ya 14 baada ya kupokea pasi ya Catous Chama na kupiga shuti kali la chini chini lililomshinda mlinda mlango Djigui Diara.

Dakika ya 45 Aziz Ki aliisawazishia Yanga kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja kufuatia Feisal Salum kufanyiwa madhambi nje ya 18.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kushambuliana kwa zamu lakini hata hivyo matokeo hayakuweza kubadilika na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Pape Sakho na Israel Patrick na Okrah na kuwaingiza Habib Kyombo, Erasto Nyoni na Kibu Denis.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER