Tumegawana Pointi na Ihefu Uwanja wa Liti

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ihefu FC uliopigwa Uwanja wa Liti mkoani Singida umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Katika mchezo huo tulianza kwa kasi huku tukitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini itabidi tujilaumu wenyewe kwani tulishindwa kuzitumia.

Wenyeji Ihefu walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Duke Abuya dakika ya 41 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Elvis Rupia.

Baada ya bao hilo tuliongeza kasi ya kutaka kusawazisha lakini Ihefu walikuwa imara kwenye ulinzi na kusababisha kwenda mapumziko wakiwa mbele.

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama alitupatia bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 71 baada ya Kibu Denis kuchezewa madhambi ndani ya 18.

Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha alifanya mabadiliko ya kuwatoa Said Ntibazonkiza, Fred Michael na Clatous Chama na kuwaingiza Pa Omar Jobe, Luis Miqussone na Willy Onana.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER