Tumegawana Pointi na APR

Mchezo wetu watatu wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya APR ya Rwanda uliopigwa katika Uwanja wa New Amaan Complex umemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu lakini zilikosa ufanisi wa kuzitumia nafasi zilizo tengenezwa.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi hasa baada ya kufanya mabadiliko ya kuingiza Jean Baleke, Willy Onana na Luis Miqussone.

Wenzetu APR walikuwa wakicheza kwa kuzuia muda mwingi wa kipindi cha pili wakionekana kuwa wengi zaidi kwenye lango lao.

Kwa matokeo hayo tumefanikiwa kutinga robo fainali ya kombe la mapinduzi na tutacheza na Jamhuri FC Januari nane.

X1: Abel, Duchu, Israel, Kennedy, Kazi, Ngoma, Jimmyson (Miqussone 45′), Kanoute (Che Malone 83′), Chilunda (Baleke 45′), Ntibazonkiza (Phiri 69′), Chalamba (Onana 45′)

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER