Tumegawana pointi Liti

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars uliopigwa Uwanja wa Liti mkoani Singida umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Deus Kaseke aliwapatia wenyeji bao lao dakika ya 11 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na kiungo Said Ndemla.

Baada ya bao hilo tuliongeza presha langoni mwa Singida lakini tulikosa utulivu wa kumalizia nafasi tulizotengeneza.

Peter Banda alitusawazishia bao hilo dakika ya 58 muda mfupi baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Jonas Mkude akimalizia pasi ya Moses Phiri.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Mkude na Kibu Denis na kuwaingiza Banda na Habib Kyombo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER