Tumegawana pointi Kirumba

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

George Mpole aliwapatia Geita bao la kwanza dakika ya 20 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Danny Lyanga akiwa ndani ya 18.

Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 22 baada ya kuumia nafasi yake ikachukuliwa na Jimmyson Mwanuke.

Kibu Denis alitusawazishia bao hilo kwa kichwa dakika ya 27 akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Rally Bwalya.

Kocha Pablo Franco aliwatoa John Bocco, Gadiel Michael, Taddeo Lwanga na Sadio Kanoute na kuwaingiza Medie Kagere, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni na Peter Banda.

Sare hii inatufanya kufikisha alama 51 baada ya kucheza mechi 24 alama 13 nyuma ya vinara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER