Tumegawana pointi Kaitaba

Kikosi chetu kimepata alama moja baada ya kupata sare ya kufungana bao moja dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa katika Uwanja wa Kaitaba.

Wenyeji Kagera walikuwa wa kwanza kupata bao la kwanza dakika ya 15 lililofungwa na mlinzi Deus Bukenya kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Ally Ramadhani ‘Kagawa’.

Baada ya bao hilo tulifanya jitihada za kusawazisha huku Kagera wakirudi wote nyuma kuzuia na kufanya mashambulizi machache ya ya kushtukiza.

Mlinzi wa kati Henock Inonga alitusawazishia bao hilo kwa kichwa dakika ya 38 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Kipindi cha pili tuliongeza mashambulizi na kuliandama lango la Kagera huku tukipoteza nafasi nyingi za mipira ya krosi ambayo ilitoka nje ya lango.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Pape Sakho na Moses Phiri na kuwaingiza Augustine Okrah na Kibu Denis.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER