Tumegawana Pointi Kaitaba

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Uwanja wa Kaitaba umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Mshambuliaji Freddy Michael alipoteza nafasi ya wazi dakika ya pili kufuatia kushindwa kumalizia pasi iliyopigwa na Mzamiru Yassin.

Ladaki Chasambi alitupatia bao la kwanza dakika ya 24 kwa shuti kali la chini chini baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na nahodha Mohamed Hussein kuzuiwa kwa kichwa na Sadio Kanoute.

Kipindi cha pili Kagera waliongeza kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni mwetu huku wakirudi wote tunapo washambulia.

Obrey Chirwa aliisawazishia Kagera bao hilo dakika ya 61 baada ya kumalizia pasi ya Deus Bukenya kufuatia mpira wa kona ya chini chini iliyopigwa na David Luhende.

X1: Ngereka, Mhilu, Luhende, Duah, Bukenya, Seseme, Mbaraka, Manyasi, Chirwa, Amza, Galiwango (Mafie 45′)

Walioonyeshwa kadi: Duah 30′ Galiwango 37′

X1: Lakred, Israel, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Babacar (Onana 77′), Balua (Jobe 87′) Mzamiru Freddy, Kanoute, Chasambi

Walioonyeshwa kadi:

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER