Tumefuzu hatua ya makundi Afrika

Licha ya sare ya kufungana bao moja dhidi ya Power Dynamos kutoka Zambia katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Azam Complex tumefanikiwa kutinga hatua ya makundi.

Tumeingia hatua hii kwa bao la ugenini kufuatia sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia, Septemba 16.

Andy Boyeli aliwapatia Power Dynamos bao la kwanza dakika ya 16 kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda Ayoub Lakred.

Baada ya bao hilo tulirudi mchezoni kutaka kusawazisha lakini Power Dynamos walirudi nyuma kuzuia na kufanya mashambulizi yakushtukiza.

Dakika ya 68 tuliopata bao la kuwasazisha baada ya mlinzi Kondwani Chiboni kujifunza akiwa katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na nahodha, John Bocco.

X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Mzamiru (Onana 58′), Chama, Ngoma, Baleke (Bocco 45′), Ntibazonkiza, Kibu (Kanoute 74′)

Walioonyeshwa kadi: Mzamiru 21′ Ntibazonkiza 44′ Lakred 90+2

X1: Mwanza, Chiboni, Soko, Makubuli, Katebe, Makwaza (Molombwa 80′), Mutale (Ngwenya 80′), Tembo, Boyeli, Zulu, Muwowo (Kalonji 60′)

Walioonyeshwa kadi: Zulu 8′ Chiboni 26′ Makubuli 40′ Boyeli 77′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER