Mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC dhidi Tabora United uliopigwa Uwanja wa KMC Complex umemalizika kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Mlinzi wa kati Che Fondoh Malone alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 13 baada ya kumalizia mpira uliopigwa na Jean Charles Ahoua.
Kiungo mshambuliaji Joshua Mutale alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 31 baada ya kupata maumivu ya mguu.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi tukifanya mashambulizi mengi langoni mwa Tabora huku wao wakiwa nyuma muda mrefu.
Valentino Mashaka alitupatia bao la pili dakika ya 68 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.
Awesu Awesu alitupatia bao la tatu dakika ya 92 akiwa ndani ya 18 kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Kibu Denis kuokolewa na walinzi wa Tabora.
X1: Camara, Kapombe (Kijili 71′), Zimbwe Jr, Che Malone, Hamza, Mzamiru (Okajepha 71′), Balua, Fernandes, Mukwala (Mashaka 57′), Ahoua (Kibu 57′), Mutale (Awesu 31′)
Walioonyeshwa kadi: Balua 75′
X1: Mandanda, Maulid, Chuku, Pemba, Bikoko, Munganga, William, Yusuph (Seseme 78′), Mhesa, Jamal, Kiberege (Moses 81′)
Walioonyeshwa kadi: Yusuph Jamal 21′