Tumefunga msimu kwa Pointi tatu muhimu nyumbani

Mchezo wetu wa mwisho wa kufungia msimu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union uliopigwa Uwanja wa Uhuru umemalizika kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Mbarak Amza aliwapatia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati dakika ya sita baada ya mlinzi Kennedy Juma kumfanyia madhambi Gerrard Gwalala ndani ya 18.

Said Ntibazonkiza alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 13 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni wavuni moja kwa moja wavuni kufuatia yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi nje ya 18.

Nahodha John Bocco alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 55 akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Shomari Kapombe.

Ntibazonkiza alitupatia bao la tatu dakika ya 73 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kapombe nje kidogo ya eneo la 18.

Matokeo haya yanatufanya kumaliza msimu tukiwa na pointi 73 alama tano nyuma ya vinara tukimaliza nafasi ya pili.

X1: Ally, Kapombe, Israel, Kennedy, Erasto, Kapama, Kyombo (Mwanuke 56′), Mkude, Bocco (Mohamed 86′), Ntibazonkiza, Kibu.

Walioonyeshwa kadi:

X1: Ndikumana, Shiga, Omary, Lawi, Kombo, Mtenje (Mkanga 72′), Gwalala (Yusuph 86′) Banda Jr (Sichela 82′) Amza (Maabad 82′), Gustapha, Vincent (Majimengi 72′)

Walioonyeshwa kadi: Omary Banda 52′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER