Tumefanya Mazoezi ya Mwisho Mo Arena

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Premiero De Agosto utakaopigiwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na jambo zuri ni kuwa hakuna aliyepata majeruhi ambayo yatamfanya kukosa mchezo huo.

Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja amejitahidi kuonyesha uwezo wake mazoezi ili kesho waaminiwe na kupata nafasi ya kuanza.

Pamoja na mambo mengine, tunaendelea kusisitiza mashabiki wawahi kufika mapema uwanjani ili kuepusha usumbufu kwa kuwa mchezo utaanza saa 10 jioni.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER