Tumefanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na Geita kesho

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena tayari kwa mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold utakaopigiwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 12 jioni.

Wachezaji wote wako tayari kwa mchezo wa kesho na wameshiriki mazoezi hayo ambapo hakuna ambaye atakosekana kwa namna yoyote.

Morali ya wachezaji ipo juu na tutaingia katika mchezo wa kesho kwa lengo moja la kupambana kuhakikisha tunashinda kwenye mechi hiyo na kuondoka na pointi zote tatu.

Tunaiheshimu Geita kwa kuwa ina kikosi imara lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya kila linalowezekana kupata alama zote tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER