Tumefanikiwa kupata pointi tatu muhimu ugenini

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja ugenini dhidi ya Vipers katika mchezo wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika Uwanja wa St. Mary’s, Katende nchini Uganda.

Mlinzi wa kati Henock Inonga alitupatia bao hilo pekee dakika ya 19 akimalizia pasi ya kichwa kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Saido Ntibanzonkiza.

Baada ya bao hilo tuliendelea kumiliki mchezo kwa kiasi kikubwa huku wenyeji Vipers wakifanya mashambulizi ya haraka lakini hata hivyo tulikuwa makini kuwakabili.

Dakika 15 za kipindi cha pili Vipers walirudi kwa kasi na kutushambulia kwa kasi lakini tulikuwa watulivu kuhakikisha hatufanyi makosa.

X1: Muderekeza, Mandela, Galiwango (Tety 66′) Mukundane, Mulondo, Sentamu, Watambala (Mwenge 45′), Anukani (Yiga 84′) Lumala (Kizza 45′), Karisa (Orit 45+2′) Yunus.

Matokeo ya leo yanatufanya kuwa na pointi tatu katika msimamo wa kundi C.

Walioonyeshwa kadi: Hakuna.

X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Joash, Henock, Kanoute, Kibu (Kyombo 81′) Mzamiru, Phiri (Erasto 60′) Ntibanzonkiza, Chama (Kennedy 90+3)

Walioonyeshwa kadi: Inonga 53′ Kibu 80′.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER