Tumefanikiwa kupata pointi tatu kwa Namungo

Kikosi chetu kimefanikiwa kupata alama tatu muhimu baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Namungo katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo ulianza kwa kasi timu zote zikishambuliana kwa zamu kutafuta bao la mapema huku tukifika zaidi langoni kwao lakini tulipoteza nafasi.

Moses Phiri alitupatia bao hilo pekee dakika ya 33 baada ya shuti lililopigwa na Mohamed Hussein kupanguliwa na mlinda mlango wa Namungo, Deogratius Munish ‘Dida’ kabla ya kumkuta mfungaji.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuliandama lango la Namungo ambao muda mwingi walikuwa wakizuia na kufanya mashambulizi machache.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya mchezaji mmoja ambapo alimtoa Augustine Okrah na kumuingiza Victor Akpan.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER