Tumefanikiwa kuifunga Wydad nyumbani

Kikosi chetu kimeibuka na ushindi wa bao moja katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo ulianza kwa kasi tukishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja huku timu zikicheza kwa tahadhari.

Jean Baleke alitupatia bao hilo pekee dakika ya 31 akimalizia pasi ya Kibu Denis kufuatia shuti la mpira wa adhabu uliopigwa na Saido Ntibazonkiza kuzuiwa na walinzi wa Wydad.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Wydad lakini mabingwa hao wa Afrika walikuwa watulivu zaidi kwenye eneo lao la ulinzi.

X1: Ally, Kapombe, Zimbwe Jr, Joash, Inonga, Kanoute, Chama, Mzamiru, Baleke (Bocco 88′) Ntibazonkiza (Sakho 80′), Kibu

Walioonyeshwa kadi: Onyango 21′

X1: El Motie, Aboulfath, Zola, Benayada (Khannouss 69′) Attiat Allah, Jabrane, Daoudi, El Hassouni, Bouhra (Moutaraji 63′), Boussefian (Haimoud 63′), Ahdad (Ellafi 83′)

Walioonyeshwa kadi: Daoudi 51′ Ahdad 84′ Zola 85′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER