Tumechukua tena ubingwa wa Kombe la Muungano

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ubingwa wa michuano ya Kombe la Muungano baada ya kuifunga Azam FC katika mchezo uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.

Kabla ya michuano hii kusimama miaka 20 iliyopita sisi tulikuwa Mabingwa na imerejea tena mwaka huu tumechukua tena ubingwa.

Tukianza mchezo kwa kasi huku tukiliandama lango la Azam na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini hata hivyo hatukuzitumia ipasavyo.

Kipindi cha kwanza tulipata kona 10 huku tukipoteza nafasi nne za wazi ambazo zingetufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa idadi hiyo lakini mlinda wa Azam alikuwa kikwazo pamoja na umakini wa wachezaji wetu.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya mashambulizi lakini hata hivyo changamoto bado ilibaki kwenye umaliziaji.

Kiungo mkabaji Babacar Sarr alitupatia bao hilo la ushindi dakika ya 76 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na nahodha Mohamed Hussein.

X1: Lakred, Israel, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Babacar, Kibu (Duchu 90+6), Ngoma, Freddy (Jobe 80′), Ntibazonkiza (Mzamiru 90′), Onana (Chasambi 88′)

Walioonyeshwa kadi:Onana 31′  Ngoma 55′ Lakred 90+5′

X1: Mustafa, Mwaikenda, Chilambo, Bangala, Funtes, Mtasigwa, Syllah, Akaminko (Zayd 80′) , Kipre Jr, Feisal, Sopu (Nado 80′)

Walioonyeshwa kadi:Sopu 74′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER