Tumechukua tatu muhimu kwa Mtibwa

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mzamiru Yassin alitupatia bao la kwanza dakika ya 38 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Augustine Okrah na kuachia shuti la chini chini lililomshinda mlinda mlango wa Mtibwa.

Dakika ya 42 mlinzi wa kati wa Mtibwa Pascal Kitenge alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Pape Sakho kisha kumkanyaga makusudi akiwa chini.

Dakika ya 48 Sakho alitupatia bao la pili baada ya kumalizia pasi safi iliyopigwa na Moses Phiri aliyepiga katikati ya walinzi wa Mtibwa.

Okrah alitupatia bao la tatu dakika ya 63 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya kifua ya Mohamed Hussein.

Nahodha wa Mtibwa Cassian Ponera alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa nyekundu dakika ya 67 kwa kumvuta jezi Okrah.

Moses Phiri alitupatia bao la nne dakika ya 63 baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Jonas Mkude kutoka katikati ya uwanja na kupiga shuti la chini chini lililomshinda mlinda mlango Hamad Kadedi.

Dakika ya mwisho ya nyongeza Sakho alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la tano kwa kichwa baada ya kumalizia krosi iliyopigwa na Gadiel Michael.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa, Okrah, Phiri, Mohamed Hussein, Phiri na Henock Inonga na kuwaingiza Peter Banda, Kibu Denis, Gadiel, Victor Akpan na Mohamed Ouattara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER