Tumechukua pointi zote za Dodoma

Kikosi chetu kimefanikiwa kuondoka na pointi zote tatu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Uhuru.

Tulianza mchezo kwa kasi huku tukiliandama lango la Dodoma lakini walikuwa imara kuhakikisha mlinda mlango wao Daniel Mgore anakuwa salama.

Jean Baleke alitupatia bao la kwanza dakika ya 43 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Hussein ambaye alipokea pasi safi kutoka kwa Clatous Chama.

Moses Phiri alitupatia bao la pili dakika ya 55 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe.

X1: Ally, Kapombe, Zimbwe Jr, Che Malone, Kennedy, Ngoma, Chama (Israel 81′), Mzamiru (Kanoute 73′), Baleke (Phiri 53′), Ntibazonkiza (Kibu 73′), Onana (Miquissone 53′)

Walioonyeshwa kadi:

X1: Mgore, Ngalema (Ngalema 69′), Justine, Mgeveke, Anderson, Mtenje, Mwana, Gustapha (Zidane 77′), Raizin (Mwaterema 69:), Martin (Hoza 51), Meshack (Paul Peter 51)

Walioonyeshwa kadi: Justine Omary 85′ Daniel Mgore 90+3.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER