Tumechukua pointi tatu zetu kwa Prisons

Kikosi chetu kimefanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu baada ya kuifunga Tanzania Prisons bao moja katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kadiri huku umiliki ukiwa mkubwa upande wetu huku Prisons wakicheza zaidi eneo lao.

Pamoja na kumiliki mchezo Prisons walifanikiwa kutuzuia na kutufanya tusitengeneze nafasi na kumfanya mlinda mlango wao kuwa salama mpaka tunakwenda mapumziko.

Medie Kagere alitupatia bao la kwanza dakika ya 68 kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Prisons kuunawa mpira ndani ya 18.

Baada ya bao hilo tuliendelea kufanya mashambulizi na kutengeneza nafasi lakini hata hivyo hatufanikiwa kuongeza la pili.

Kocha Msaidizi Seleman Matola, aliwatoa Mzamiru Yassin, Clatous Chama, Hassan Dilunga, Rally Bwalya na Kagere kuwaingiza Pape Sakho, John Bocco, Jimmyson Mwinuke, Jonas Mkude na Chris Mugalu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER