Tumechukua pointi tatu za Singida FG

Mchezo wetu wa pili wa Kombe la Mapinduzi uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex umemalizika kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kutengeneza nafasi lakini safu za ulinzi zilikuwa imara kuhakikisha nyavu zao haziguswi.

Willy Onana alitupatia bao la kwanza dakika ya 46 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi nje kidogo ya 18.

Luis Miqussone alitupatia bao la pili kwa shuti kali la mguu wa kushoto dakika ya 58 baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe.

X1: Ally, Kapombe, Israel, Kennedy, Che Malone, Abdallah (Mussa 45:)(Chilunda 81′), Phiri (Miqussone 45′), Kanoute, Bocco (Baleke 45′), Ngoma, Onana (Karabaka 81′)

Walioonyeshwa kadi: Ally 72′ Mohamed Mussa 76′ Kanoute 83′

X1: Ibrahim, Kijili, Mbegu (Kadikilo 68′), Onyango, Carno, Kagoma, Kaseke, Chukwu, Rupia (Ambundo 68′), Kyombo (Kazadi 68) , Abuya (Kagere 68′)

Walioonyeshwa kadi: Kyombo, Kijili 50′ Mbegu 68′ Carno 80′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER