Tumechukua Pointi tatu za Ihefu

Timu yetu imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Jean Baleke alitupatia bao la kwanza dakika ya 12 baada ya kuinasa pasi iliyopigwa na Joseph Mahundi kwenda kwa mlinda mlango Fikirini Bakari.

Ismail Mgunda aliisawazishia Ihefu bao hilo dakika ya 25 baada ya shuti kali lililopigwa na Rajabu Athumani kuokolewa na mlinda mlango Ally Salim kabla ya kumkuta mfungaji.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Ihefu lakini walikuwa imara huku wakirudi wote nyuma kuzuia.

Moses Phiri alitupatia bao la pili dakika ya 65 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wawili wa Ihefu kufuatia kupokea pasi safi kutoka kwa Luis Miquissone.

Ushindi wa leo unatufanya kufikisha pointi 18 baada ya kushinda mechi zote sita za Ligi tulizocheza mpaka sasa.

X1: Ally, Kapombe (Israel 89′), Zimbwe Jr, Che Malone, Henock, Ngoma, Chama (Chilunda 75′), Kanoute (Mzamiru 75′), Baleke (Phiri 45′), Ntibazonkiza, Kibu (Miquissone 45′)

Walioonyeshwa kadi:

X1: Mapala, Kunambi, Mwakinyuke, Nyoso, Mwihambi, Akpan (Mwashilindi 65′) Manyasi, Tigere (Saadun 54′), Mgunda (Ilanfya 54′), Rajabu (Amza 65′), Mahundi

Walioonyeshwa kadi: Tigere 37′ Saadun 83′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER