Tumechukua pointi tatu muhimu kwa Polisi

 

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Tulianza mchezo kwa kasi na kuliandama lango la Polisi katika dakika 20 za mwanzo ili kutafuta bao la mapema lakini tulikosa utulivu katika eneo la mwisho.

Nahodha John Bocco alitupatia bao la kwanza dakika ya 32 baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Shomari Kapombe kutoka upande wa kulia.

Moses Phiri aliongeza bao la pili dakika ya 42 baada ya kupokea mpira kutoka kwa Clatous Chama ndani ya 18 ambaye alimlamba chenga mlinzi wa Polisi kabla ya kutoa pasi.

Phiri tena alitupatia bao la tatu dakika ya 52 baada ya kupokea mpira kutoka kwa Chama ambaye aliwazidi ujanja walinzi wa Polisi kabla ya kutoa pasi.

Zuberi Khamisi aliipatia Polisi bao la kufutia machozi dakika ya 90 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Ambrose Awio kutokea upande wa kushoto.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Gadiel Michael na Bocco na kuwaingiza Kennedy Juma na Kibu Denis.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER