Tumechukua pointi tatu kwa Wydad

Kikosi chetu kimeondoka na pointi zote tatu nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wydad Casablanca katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zikisomana lakini Wydad walifanya mashambulizi makali mawili dakika ya 28 na 32 lakini mlinda mlango Ayoub Lakred alikuwa imara na kuondoa hatari zote.

Willy Onana alitupatia bao la kwanza dakika ya 35 kwa shuti kali nje kidogo ya 18 baada ya kumalizia pasi ya kifua iliyopigwa na Kibu Denis.

Dakika mbili baadae Onana alitupatia bao la pili baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin.

Matokeo haya yametufanya kufikisha pointi tano tukipanda hadi nafasi ya pili tukiwa nyuma kwa alama mbili dhidi ya vinara ASEC Mimosas.

X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr, Che Malone, Henock, Ngoma, Kibu (Duchu 67′), Mzamiru (Abdallah 79′), Beleke (Kennedy 79′), Chama (Bocco 60′), Onana (Israel 60′)

Walioonyeshwa kadi: Mzamiru 47′ Israel 80′ Lakred 89′ Abdallah 90+8.

X1: El Motie, Serrhat (Bahri 75′), Abdulfath, Haimoud, El Idriss, Harkass, Draoui, Lahtimi (Ounnajem 45′),Amloud, (Moutaraji 45′) Sambou, Bouhra

Walioonyeshwa kadi:

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER