Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa katika Uwanja wa Jamhuri umemalizika kwa kuibuka na ushindi wa bao moja.
Mchezo ulianza kwa kasi huku tukifanya mashambulizi langoni mwa Dodoma lakini hata hivyo tulikosa umakini wa kutumia nafasi tulizopata.
Jean Charles Ahoua alitupatia bao la kwanza kwa mkwaju penati dakika ya 62 baada ya nahodha Mohamed Hussein kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Baada ya bao hilo tuliendelea kuliandama lango la Dodoma na kufanya mashambulizi mengi langoni Dodoma.
Katika mechi hiyo kiungo mshambuliaji Deborah Fernandez amechaguliwa nyota bora wa mchezo.
X1: Ngeleka, Mhilu Jr, Dissan, Onyango, Nsata, Hoza, Apollo, Mwana, Waziri (Mwaterema 68′) Ajibu (Peter), Kipagwile (Lusajo 67′)
Walioonyeshwa kadi: Hoza 60′ Galiwango 88′
X1: Camara, Kijili (Kapombe 58′), Zimbwe Jr, Che Malone, Hamza, Ngoma (Okajepha 65′), Kibu (, Fernandez, Ateba, Mukwala (Awesu 45′), Ahoua (Nouma 79′)
Walioonyeshwa kadi: Kapombe 72′ Che Malone 77′