Tumezipata alama tatu za nyumbani dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku ukichezwa zaidi katikati ya uwanja mashambulizi yakiwa machache yaliyofika kwa walinda milango.
Sadio Kanoute alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 19 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Ladaki Chasambi.
Baada ya bao hilo tuliongeza kasi ya kutafuta mengine zaidi lakini hata hivyo tulipoteza umakini wa kuzitumia.
Edwin Balua alitupatia bao la pili dakika ya 76 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin.
Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 53 tukiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 24.
X1: Lakred, Israel, Zimbwe Jr, Kennedy Che Malone, Ngoma (Hamis 86′), Balua (Karabaka 79′), Mzamiru, Freddy (Jobe 79′), Kanoute, Chasambi (Duchu 90+2)
Walioonyeshwa kadi: Jobe 88′
X1: Noble, Maulid, Madirisha, Pemba, Bikoko, Milandu (Jarome 83′), Daniel (Nakibinge 53′), Najim, Okutu (Lembo 87′), Kalumba, Mbombo
Walioonyeshwa kadi: Madirisha 52′ Mbombo 80′ Banza 90+1