Tumechangia Wahanga wa mafuriko Hanang

Klabu yetu leo imekabidhi msaada kwa ajili ya wahanga wa mafuriko na maporomoko yalitokea katika Wilaya ya Hanang mkoani Manyara mwishoni mwa juma lililopita.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ amemkabidhi msaada huo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dr. Damas Ndumbaro ambaye ataepeleka kwa wahusika huko Hanang.

“Kwa niaba ya Rais wa heshima Mohamed Dewji, Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti wapenzi na Wanachama wa Simba tunapenda kutoa pole nyingi kwa wahanga wa mafuriko na maporomoko huko Hanang.

“Wengi wa wahanga hawa ni wapenzi wa soka na sisi kama klabu tunaungana nao kwenye kipindi hiki kigumu,” amesema Try Again.

Akipokea msaada huo, Waziri Dk. Ndumbaro ameushukuru Uongozi wa klabu kwa kuona umuhimu wa kuwachangia wenzetu wa Hanang huku akiwaomba wadau wengine kuguswa na kutoa kwa ajili ya wahanga.

“Kwa niaba ya Serikali tunaushukuru Simba kwa mchango huu mkubwa kwa ajili ya ndugu zetu wa Hanang waliopata matatizo huko Hanang, watafarijika sana wakiona msaada huu kutoka kwetu,” amesema Dk. Ndumbaro.

Msaada tuliotoa ni unga, mchele, mafuta ya kupikia, sabuni maji ya kunywa ambayo tumejaza gari mbili.

Katika zoezi hilo la kukabidhi msaada huo limehidhuriwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo, Neema Msitha.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER