Tumeanza vizuri mzunguko wa pili NBC

Kikosi chetu kimeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Pape Sakho alitupatia bao la kwanza dakika ya nane kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe kutoka upande wa kulia.

Dakika ya 13 Mzamiru Yassin alitupatia bao la pili kwa kichwa akimalizia mpira krosi uliopigwa kwa ustadi na Kapombe.

Clatous Chama alitupatia bao la tatu dakika ya 18 baada ya kuwalamba chenga walinzi wawili wa Biashara Boniface Maganga na Abdulamajid Mangalo kufuatia pasi safi ya Sakho.

Kapombe alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 28 baada ya kugongwa kichwani na mshambuliaji Atupele Green.

Kipindi cha pili tulitengeneza nafasi nyingi huku tukifanya mashambulizi lakini hata hivyo ufanisi wetu kwenye kuzitumia haukuwa wa kutosha.

Dakika ya 92 Medie Kagere alikosa mkwaju wa penati uliodakwa na mlinda mlango wa Biashara James Ssetuba baada ya Bernard Morrison kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kocha Pablo Franco aliwatoa John Bocco, Sakho, Mohamed Hussein, Henock Inonga na kuwaingiza Kagere, Morrison, Gadiel Michael na Kennedy Juma.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER