Tumeanza msimu kwa ushindi mnono

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tulianza mchezo huo kwa kasi tukiliandama lango la Geita dakika 15 za mwanzo lakini tulikosa umakini katika eneo la mwisho.

Augustine Okrah alitupatia bao la kwanza dakika ya 37 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja kwa mguu baada ya Clatous Chama kufanyiwa madhambi nje ya 18.

Moses Phiri alitupatia bao la pili dakika ya 61 baada ya kupokea pasi safi kutoka Chama akiwa ndani ya 18.

Chama alitupatia bao la tatu kwa mkwaju wa penati dakika ya 81 baada ya Okrah kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kocha Zoran Maki aliwatoa Jonas Mkude, Phiri, Peter Banda, Pape Sakho na Chama na kuwaingiza Okrah, Dejan Georgejivic, Mzamiru Yassin, Kibu Denis na Nelson Okwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER