Tumeanza kwa Ushindi Sudan

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana mchezo uliopigwa Uwanja wa Al Hilal nchini Sudan.

Katika mchezo huo Steven Mukwala aliwapatia Kotoko bao la kwanza dakika ya tisa baada ya walinzi wetu kuchelewa kuondoa hatari.

Augustine Okrah alitusawazishia bao hilo dakika ya 19 baada ya kumalizia pasi ya mlinzi wa kulia Israel Patrick.

Pape Sakho alitupatia bao la pili dakika ya 26 baada ya kuwalamba chenga walinzi wa Kotoko na kupiga shuti la chini chini lililomshinda mlinda mlango.

Clatous Chama alitupia la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya Moses Phiri kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Chama alitupatia bao la nne dakika ya 55 baada ya kumlamba chenga mlinzi mmoja wa Kotoko kufuatia kupokea pasi kutoka kwa Peter Banda.

Steven Amankona aliwapatia Kotoko bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 78 baada ya Nassor Kapama kufanya madhambi ndani ya 18.

Kocha Zoran Maki aliwatoa Mohamed Ouatara, Phiri, Chama, Sakho na Ally Salim na kiwaingiza Peter Banda, Dejan Georgijevic, Jimmyson Mwanuke, Nelson Okwa na Ahmed Feruz.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER