Mechi yetu ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli iliyopigwa katika Uwanja wa Kimataifa wa Tripoli umemalizika kwa sare ya bila kufungana.
Mchezo ulianza kwa kasi huku wenyeji Al Ahli Tripoli wakishambulia kwa kasi lakini safu yetu ya ulinzi ilikuwa imara kuhakikisha Moussa Camara anakuwa imara.
Kuanzia dakika ya 20 tulitawala mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Al Ahli Tripoli ingawa hatukuweza kuwa makini kwenye kutoa pasi za mwisho.
Kipindi cha pili wenyeji Tripoli walirudi kwa kasi na kuongeza presha kwenye lango letu lakini tulikuwa makini kuhakikisha tunalinda na kutoruhusu bao.
Baada ya mchezo wa leo kumalizika tunarejea nyumbani kujipanga na mechi ya marudiano itakayopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 22.
X1: Camara, Kapombe, Zimbwe, Jr Che Malone, Hamza, Kagoma, Balua (Okajepha 67′) Fernandez (Ngoma 81′), Ateba (Mashaka 60′), Ahoua (Chamou 81′), Mutale (Kibu 67′)
Walioonyeshwa kadi: Kibu 91+1