Tumeanza kwa Pointi tatu Mapinduzi Cup

Mchezo wetu wa kwanza wa michuano ya Mapinduzi tuliocheza dhidi ya JKU katika Uwanja wa New Amaan Complex umemalizika kwa ushindi wa mabao 3-1.

Moses Phiri alitupatia bao la kwanza dakika ya nane baada ya kupokea ya kupokea pasi safi kutoka kwa Luis Miqussone.

Mshambuliaji Neva Kaboma aliisawazishia JKU bao hilo dakika ya 42 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu na kupiga shuti lililomgonga Che Malone na kumchanganya mlinda mlango Ayoub Lakred.

Mohamed Hassan alijifunga na kutupatia bao la pili dakika ya 64 katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Miqussone.

Saleh Karabaka alitupatia bao la tatu dakika ya 65 muda mfupi baada ya kuingia na kupiga shuti liliomshinda mlinda mlango Enock Gerard.

X1: Lakred, Kapombe, Duchu, Kazi, Che Malone, Ngoma, Mwanuke (Onana 45′), Kanoute, Chilunda (Mussa 45′), Phiri (Baleke 45′), Miqussone (Kalabaka 64′)

Walioonyeshwa kadi:

X1: Enock (Haji Ally 69′), Yakubu (Ubwaka 55′), Suwed, Mohamed, Shaban, Hassan (Antwi 68′), Saleh, Adam, Nassor, Ahmed (Machano 56′), Neva

Kazi 16′ Chilunda 27′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER