Tumeacha alama zote tatu Sokoine

 

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mchezo ulianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta bao la mapema kujihakikishia ushindi lakini kulikosekana umakini kwenye eneo la mwisho.

Walinda milango Beno Kakolanya na yule wa Prisons Hussein Abel waliokoa michomo ya hatari ambayo kama wasingekuwa makini nyavu zao zingetikisika mapema kipindi cha kwanza.

Nahodha Benjamin Asukile aliwapatia Prisons bao la kwanza dakika ya 53 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Jeremiah Juma kabla ya kuunganishwa na Mudathir Abdallah na kuokolewa na Kakolanya kabla ya kumkuta mfungaji.

Kocha Seleman Matola alifanya mabadiliko ya mchezaji mmoja ambapo alimtoa Taddeo Lwanga na kumuingiza Mzamiru Yassin.

Mchezo huu ni wa kwanza wa Matola kupoteza tangu awe kaimu kocha mkuu baada ya kushinda mechi tatu za mwanzo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER