Tulipotoka hadi kufika Nusu Fainali ASFC

Kikosi chetu leo saa 9:30 Alasiri kitashuka katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona kuikabili Azam FC katika mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Kabla ya mchezo wa leo tumecheza mechi nne ambazo zimetupa tiketi ya kukutana na Azam kwenye mechi ya nusu fainali.

Safari yetu ilipoanzia Hadi kufika leo…..

Hatua ya 64…………

Simba 8-0 Eagle FC

Mchezo wetu wa kwanza wa ASFC ulikuwa dhidi ya Eagle FC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Disemba 10, 2022 ambao ulikuwa hatua ya 64 bora na tulishinda mabao 8-0.

Mabao yetu yalifungwa na

Moses Phiri ⚽⚽⚽⚽
Clatous Chama ⚽⚽
Habib Kyombo ⚽
Pape Sakho ⚽

Hatua ya 32……………

Simba 1-0 Coastal Union

Mchezo wetu wa hatua ya 32 bora dhidi ya Coastal Union ulipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Januari 28, 2022 na tulifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja.

Bao letu lilifungwa na

Sadio Kanoute ⚽

Hatua ya 16…………….

Simba 4-0 African Sports

Mchezo wetu wa hatua ya 16 bora ulipigwa Machi 2, 2023 katika Uwanja wa Uhuru na tuliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Mabao yetu yalifungwa na

Jean Baleke ⚽
Kennedy Juma ⚽
Mohamed Mussa ⚽
Jimmyson Mwanuke ⚽

Robo fainali………………….

Simba 5-1 Ihefu

Mchezo wetu wa robo fainali uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Aprili 7, 2023 na tuliibuka na ushindi wa mabao 5-1.

Mabao yetu yalifungwa na

Jean Baleke ⚽⚽⚽
Saido Ntibazonkiza ⚽
Pape Sakho ⚽

N.B

Mpaka tunaingia kwenye mchezo wa leo wa nusu fainali tayari tumefunga mabao 18 tukiwa tumeruhusu bao moja.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER