‘Tuko tayari kupambania alama tatu kwa KMC’

Kikosi chetu leo Ijumaa Desemba 24, kitashuka katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora kwa ajili ya kupambania alama tatu muhimu dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Pamoja na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wanaougua hivyo kushindwa kufanya maandalizi vizuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunarejea jijini Dar es Salaam na alama zote tatu.

Wachezaji wote 24 tuliosafiri nao wapo kamili na jana walifanya mazoezi ya mwisho tayari kwa mtanange wa leo.

KOCHA PABLO

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema mchezo utakuwa mgumu kwetu kutokana na kukosa muda wa kujiandaa baada ya wachezaji wengi kuugua siku chache zilizopita na kushindwa kufanya mazoezi ya pamoja.

Pablo amesema KMC ni timu nzuri na inacheza kwa ushiriakiano mkubwa uwanjani kuanzia katika ulinzi, viungo hadi washambuliaji hivyo tutaingia kwa tahadhari na kuwaheshimu.

“Mechi itakuwa ngumu KMC ni timu nzuri, hatujapata muda mrefu wa kujiandaa kuelekea mchezo huu lakini Simba ni kubwa hivyo tutajipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Pablo.

MKUDE AWAITA MASHABIKI

Kiungo, Jonas Mkude amewaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kutoa sapoti kwa wachezaji ili kuhakikisha alama tatu zinapatikana.

“Mimi nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani, sisi wachezaji tupo tayari kupambana kuhakikisha tunawapa furaha kwa kupata ushindi,” amesema Mkude.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER