Tuko tayari kumalizia tulipoishia Botswana

Leo jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kikosi chetu kitashuka dimbani kuikabili Jwaneng Galaxy kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mchezo wa leo ni marudiano kutokana na ule wa kwanza uliofanyika jijini Gaborone Jumapili iliyopita ambapo tulifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Katika mchezo wa kwanza tumefanya kazi nusu na kurudi na faida ya mabao mawili ya ugenini na iliyobaki tutaimaliza leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Mshindi wa jumla katika mchezo wa leo atatinga moja kwa moja hatua ya makundi ya michuano hiyo huku sisi tukiwa na faida zaidi kutokana na ushindi wa ugenini tuliopata.

Kocha Msaidizi Thierry Hitimana, amesema maandalizi yote ya mchezo yamekamilika na masuala yote ya ufundi yako vizuri kilichobaki ni wachezaji kuyatimiza uwanjani.

“Tunachoangalia kwa sasa ni kupata nafasi ya kuingia hatua ya makundi, tumejipanga kuimarisha kiwango cha uchezaji wetu ili kutoa burudani kwa mashabiki watakaojitokeza,” amesema Hitimana.

TAARIFA YA KIKOSI

Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri morali ipo juu na wamefanya mazoezi ya mwisho jana kujiandaa na mchezo.

MUGALU KUIKOSA JWANENG

Mshambuliaji Chris Mugalu ndiye mchezaji pekee ambaye ataukosa mchezo wa leo kutokana na kuendelea kuuguza jeraha la mguu.

Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho yeye amepona na amerejea mazoezini toka juzi na benchi la ufundi litaamua kama watamtumia au la.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER