Tuko Mkwakwani kuikabili Coastal

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga kuikabili Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Maandalizi ya mchezo yamekamilika, kikosi kiliwasili juzi jijini hapa na jana kimefanya mazoezi ya mwisho Mkwakwani kujiweka sawa kabla ya mechi ya leo.

Tutaingia katika mchezo wa leo kwa kuiheshimu Coastal na tunajua ni timu nzuri inacheza nyumbani kwa hiyo tumechukua tahadhari zote na lengo ni kurudi nyumbani na pointi zote.

KOCHA MGUNDA AFUNGUKA

Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema wachezaji wote 22 waliopo hapa wapo kwenye hali nzuri tayari kuipigania timu kupata alama tatu muhimu ugenini leo.

Mgunda ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu kwani Coastal watapambana kuhakikisha wanashinda katika uwanja wao wa nyumbani lakini tumejiandaa kikamilifu kuwakabili.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, baada ya mechi yetu dhidi ya Polisi Tanzania kikosi kilirudi Dar es Salaam na siku iliyofuata tulianza mazoezi kwa ajili ya mchezo wa leo. Tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kikamilifu kupata ushindi,” amesema Mgunda.

KAULI YA ALLY SALIM

Mlinda mlango, Ally Salim amesema kwa upande wao wachezaji wapo tayari kufuata maelekezo yote watakayopewa na walimu lengo likiwa ni kuhakikisha tunarejea Dar es Salaam na alama zote tatu.

“Sisi kama wachezaji tuko tayari kuhakikisha tunapambana na kufuata maelekezo ya walimu kwa kuwa lengo letu ni kushinda,” amesema Salim.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER