Tukirudi kwenye Ligi tunaanza na Tabora United

Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imetoa ratiba ya mechi za Ligi Kuu ya NBC ambayo itaendelea mapema mwezi ujao.

Awali TPLB ilisitisha Ligi Kuu kwa ajili ya kupisha michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) ambayo ilikuwa imepangwa kuanza Februari Mosi katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kabla kuahirishwa mpaka Agosti.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi mchezo wetu wa kwanza wa mzunguko wa pili utakuwa Februari 2 dhidi ya Tabora United ambao utapigwa katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Mchezo wetu wa ‘Dabi ya Kariakoo’ utapigwa Machi 8 wakati ule wa ‘Dabi ya Mzizima’ dhidi ya Azam FC utapigwa Februari 24.

Hii hapa ratiba ya mechi tano za kwanza

Tabora United Vs Simba Februari 2, Ali Hassan mwinyi

Fountain Gate Vs Simba Februari 6, Tanzanite Kwara

Simba Vs Tanzania Prisons Februari 11, KMC Complex

Simba Vs Dodoman Jiji Februari 15, KMC Complex

Namungo FC Vs Februari 19, Simba Uwanja wa Majaliwa

Simba Vs Azam FC Februari 24, KMC Complex.

Yanga Vs Simba Machi 8, Benjamin Mkapa

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER