Try Again mtaja Rais Samia, Mashabiki ushindi wa Horoya

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa motisha anayotoa katika michuano ya Ligi ya Afrika kwa timu za hapa nyumbani.

Try Again amesema kiasi cha Sh. 5,000,000 anazotoa Rais Samia kwa kila bao linalofungwa kimeongeza morali na kuwafanya wachezaji kujiona na deni kubwa kwa nchi.

Try Again pia ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo chini ya Waziri Pindi Chana kwa ushirikiano wanautupa mpaka kufika hatua.

Aidha Try Again pia amewashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu na hicho kimechangia mpaka leo tumefanikiwa kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, wachezaji na wote mlioko hapa kwa niaba ya Rais wa heshima na muwekazaji Mohamed Dewji ‘Mo’ tunakushukuru Waziri, hii ndio Simba kwenye shughuli hizi wengine wanaiga lakini sisi ndio waanzilishi.

“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Saluhu kwa kueendele kutupa sapoti kupitia motisha anayotoa kwa kila bao linalofungwa.

“Tunaishukuru Wizara yetu na mashabiki wetu mnavyotusapoti tuendelee kuwa wamoja tuzidi kufanya vizuri,” amesema Try Again.

Waziri Chana ametukabidhi pesa taslimu Sh. 35,000,000 kutoka kwa Dk. Samia kufuatia kupata ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER