Timu yawasili Zanzibar yafanya mazoezi ya mwisho

Baada ya kuwasili salama Visiwani Zanzibar mchana kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa nje wa Amaan kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya JKU.

Kikosi kimeondoka jijini Dar es Salaam mchana na baada ya kufika wachezaji walipumzika kabla ya usiku kuelekea uwanjani kwa ajili ya mazoezi tayari kwa maandalizi ya mtanange wa kesho.

Wachezaji wote 20 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho.

Mchezo wetu dhidi ya JKU utapigwa kesho saa 2:15 usiku katika Uwanja wa New Amaan Complex.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER