Timu yawasili salama Visiwani Zanzibar

Kikosi chetu kimewasili salama Visiwani Zanzibar tayari kwa mechi mbili za kirafiki kufuatia mwaliko kutoka Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) kipindi hiki ligi ikiwa imesima kupisha mechi za kalenda ya FIFA.

Kikosi kimeondoka jijini Dar es Salaam jioni kikiwa na wachezaji 21, benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi.

Jumapili saa 2:15 usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Amani kucheza na Malindi katika mchezo wa kwanza wa kirafiki.

Jumatano Septemba, 28 tutacheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Kipanga FC katika Uwanja huo huo wa Amani saa 2:15 usiku.

Kesho timu itafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na Malindi kabla ya kushuka dimbani Jumapili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER