Kikosi chetu kimewasili salama nchini ya Uganda tayari kwa mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers utakaopigwa Jumamosi.
Kesho kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa St. Mary’s ambapo mchezo wetu utapigwa siku ya Jumamosi.
Hali ya wachezaji ni nzuri na morali ipo juu na kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anapambana kuipigania timu kupata ushindi dhidi ya Vipers.
Mchezo wetu dhidi ya Vipers utapigwa Jumamosi katika Uwanja wa St. Mary’s wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15,000 kuanzia saa moja usiku.