Timu yawasili salama Morocco

Kikosi chetu kimewasili salama nchini Morocco jioni hii tayari kuanza maandalizi ya mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane.

Timu imefika katika Jiji la Casablanca ambapo itaweka kambi ya siku tatu kabla ya kwenda katika mji wa Berkane ambapo mchezo wetu utafanyika.

Wachezaji, benchi la ufundi pamoja na viongozi walioambatana na timu wote wako katika hali nzuri kiafya.

Mchezo wetu dhidi ya Berkane utapigwa Jumapili saa nne usiku kwa saa za nyumbani.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER