Timu yawasili salama Libya

Kikosi chetu kimewasili salama nchini Libya tayari kwa mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli utakaopigwa Jumapili Septemba 15.

Kikosi kimeondoka Uturuki asubuhi na kuelekea Libya kufuatia safari ya jana ya kutokea jijini Dar es Salaam.

Wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa Ally Salim Mohamed Hussein, Edwin Balua na Moussa Camara tayari wamejiunga na wenzao.

Baada ya kuwasili Libya wachezaji watapata saa chache za kupumzika na jioni wataanza programu ya mazoezi.

Tutakuwa na siku tatu za kufanya mazoezi nchini Libya kabla ya kukutana na Al Ahly Tripoli ili kuwafanya wachezaji wetu kuzoea hali ya hewa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER