Timu yawasili salama Guinea

Kikosi chetu kimewasili salama nchini Guinea saa 11 jioni ambapo nyumbani Tanzania ni saa mbili usiku tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya FC.

Kikosi kimefika katika mji wa Conakry ambapo mchezo wetu wa Jumamosi utafanyika saa 10 jioni kwa saa Guinea ambapo nyumbani itakuwa itakuwa saa moja usiku.

Wachezaji wote 24 waliosafiri wapo sawa kiafya ukiacha uchovu wa safari ndefu angani lakini wapo kamili kuipigania Simba.

Kesho kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa (Stade General Lansana Conte) ambao utatumika kwa mechi kwa mujibu wa kanuni za CAF ili kujiweka sawa kwa pambano la Jumamosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER