Timu yatua salama Sudan

Baada ya saa kadhaa angani hatimaye kikosi chetu kimewasili salama nchini Sudan tayari kwa mechi mbili za kirafiki za kimataifa kutokana na mwaliko tuliopata kutoka Al Hilal.

Kikosi kiliondoka jijini Dar es Salaam saa 10 alfajiri na kuwasili Khatoum saa sita mchana ambapo wachezaji wamepewa mapumziko ya saa chache.

Wenyeji wetu Al Hilal wametupokea vizuri kutoka tulipowasili Uwanja wa Ndege hadi hoteli tuliyofikia na kila kitu ambacho tunastahili kupata.

Saa 11 jioni ambapo huko nyumbani itakuwa saa 12 kikosi kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili (recovery) baada ya uchovu wa safari.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER